Uongozi wa Hawza umesisitiza kuwa lengo kuu la maadhimisho haya ni kuendeleza utamaduni wa kumkumbuka Bibi Zahra (sa) na kufuata nyayo zake katika kujenga jamii yenye maadili, elimu, na imani imara.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Wanafunzi mabinti wa Hawza ya Hazrat Zainab (sa), iliyoko Kigamboni – Dar es Salaam, wameendelea na majalisi za maombolezo na ukumbusho wa shahada ya Bibi Fatima Al-Zahra (sa), binti wa Mtume Mtukufu Muhammad (saw).
Majlisi hizo, ambazo zimekuwa zikiandaliwa kwa nidhamu na hisia za kiroho, zinahusisha hotuba za kielimu, usomaji wa riwaya za maisha ya Bibi Zahra (sa), na mawaidha kuhusu nafasi ya mwanamke Muislamu katika Uislamu wa kweli.
Wahadhiri na wanafunzi kwa pamoja wamekuwa wakitumia majlisi hizi kama fursa ya kujifunza maadili, unyenyekevu, na uthabiti wa kiimani uliodhihirishwa na Bibi Fatima (sa) katika maisha yake, hususan katika kulinda mafundisho ya Mtume (saw) na haki za Ahlulbayt (as).
Aidha, majlisi hizo zimeambatana na kisomo cha Qur’an, marsiya, na dua maalum, ambapo washiriki wameonyesha upendo, heshima, na huzuni ya dhati kwa tukio hili tukufu la kihistoria.
Uongozi wa Hawza umesisitiza kuwa lengo kuu la maadhimisho haya ni kuendeleza utamaduni wa kumkumbuka Bibi Zahra (sa) na kufuata nyayo zake katika kujenga jamii yenye maadili, elimu, na imani imara.

Your Comment